KOCHA MWAMAJA AFUKUZA TANZANIA PRISON - LEKULE

Breaking

5 Mar 2015

KOCHA MWAMAJA AFUKUZA TANZANIA PRISON


Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Davida Mwamaja amebwaga manyanga ndani ya kikosi hicho, imefahamika.
Kutokana na mwenendo mbaya wa timu yake ikiwa mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, Mwamaja amesema ameamua kung’atuka katika klabu hiyo.

“Nimeona hali ni mbaya katika timu ndiyo maana nimeamua nikae nje ili watafue namna ya kuinusuru kubaki katika ligi,” amesema kocha huyo aliyewahi kuinoa Simba SC 1999 wakati Mtibwa Suga FC wakitwaa taji la kwanza la Tanzania Bara.

Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Prisons zilizoufikia mtandao huu, zimedai kuwa kocha huyo ametimuliwa na nafasi yake imechukuliwa na Mbwana Makata aliyewahi kuwa kocha wa JKT Ruvu na Rhino Rangers FC ya Tabora iliyoshuka daraja msimu uliopita.

Mwamaja anakuwa kocha wa pili kutimuliwa ndani ya siku nne baada ya uongozi wa Azam FC kumfungashia virago Mcameroon Joseph Omog mara tu baada ya kikosi chaop kutolewa kwa jumla ya mabao 3-2 dhidi ya El-Merrikh FC ya Sudan katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika mwaka huu.

No comments: