Kwa kuliwa Ush. 500,000 wakati Monaco ilipoichapa Arsenal 3-1 katika mechi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano, Deus Ruhinda mkazi wa Kakiika katika wilaya ya Mbarara alifanya kisichofikirika kwa kujinyonga.
Mashuhuda wa kifo hicho wamekaririwa na mtandao wa Kawowo Sports wakieleza kuwa kimetokana na kuliwa katika mchezo wa kubahatisha ‘betting’.
Marehemu (Ruhinda) aliyekuwa akifanya kazi wilayani Kasese, Uganda, alichukua uamuzi huo mgumu wa kuakatisha maisha yake baada ya kuliwa Ush. 500,000 katika mechi hiyo.
Marehemu alikuwa dereva wa pikipiki za biashara (bodaboda) na pesa aliyoiweka bondi ilikuwa ya bosi wake (mmiliki wa pikipiki).
Baada ya kuliwa, alirudi nyumbani kwao alikozaliwa, ambako alikuwa na miaka sita bila kurejea, na kujinyonga.
Imeelezwa kuwa baada ya kufika nyumbani na kueleza tukio hilo huku akijuzwa kuhusu kufariki kwa wazazi wake, bibi yake, Nalongo Geturiida, alimfokea kwa kucheza michezo ya kubahatisha.
Baada ya kufokewa na bibi yake, imelezwa kuwa alikasirika zaidi kusikia bibi yake huyo hakuwa tayari kumsaidia kwa lolote.
Baadaye Ijumaa, Ruhinda akakutwa amejinyonga kwenye mti wa familia yao uliomo ndani ya shamba lao la ndizi.
Kifo cha Ruhinda ni mwendelezo wa vifo vingi vya kujinyonga, kuchanganyikiwa na matukio mengine yanayotokana na michezo ya kubahatisha kutokana na matokeo ya michezo mbalimbali ulimwenguni.
Stori za mtu kuweka rehani nyumba yake kwa nia ya kupata fedha nyingine nyingi kwa ‘betting’ na wanaume kuweka rehani wake zao na watoto ni vya kawaida katika nchi za Kenya na Uganda.
Kicho cha aina hiyo kilitokea kwa mara ya mwisho Septemba mwaka jana wakati Fahad Musana, wa Uganda alipokufa kutokana na goli la Lampard dhidi ya Man United.
No comments:
Post a Comment