Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Mpwapwa kwenye uwanja wa mikutano Mnarani ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa ahadi zilizoahidiwa na CCM zitatekelezwa kama ilivyopangwa.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa akihutubia wananchi wa Mpwapwa mjini na kuwaambia katika uongozi wake atawapa nafasi wale watu wanaotakiwa na wananchi wenyewe kuwaongoza na kusema hakutokuwa na makosa ya kukata majina.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa akiwahutubia wananchi wa Mpwapwa mkoani Dodoma na kuwaambi wawe makini na baadhi ya vyama vya siasa vinavyo andaa vijana kuingia msituni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia shamba la karanga la Bi. Anna Mlewa, wengine ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Chiku Galawa (kulia).
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Mzee Robert Matonya mkazi wakijiji cha Kisokwe wilayani Mpwapwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea tofali kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa wakati wa kushiriki ujenzi ya zahanati ya Kisokwe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wanafunzi lililoungua moto mapema mwanzoni mwa mwaka.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi kwenye ofisi ya CCM tawi la Mpwapwa mjini.
No comments:
Post a Comment