Keshi arejea licha ya kulazwa na Uganda - LEKULE

Breaking

27 Mar 2015

Keshi arejea licha ya kulazwa na Uganda

Stephen Keshi atarejea kama mkufunzi wa Super Eagles ya Nigeria shirikisho la soka la taifa hilo NFF limetangaza.
Kocha huyo mkongwe 53, aliyeiongoza Super Eagles kutinga raundi ya pili ya kombe la dunia lililofanyika mwaka uliopita.
Alilazimika kuacha kazi baada ya kurejea nyumbani kutoka Brazil akidai kupewa kandarasi mpya.
Hata hivyo mzozo wa uongozi katika NFF ililazimu mazungumzo hayo kuendelea kwa kipindi kirefu lakini sasa rais wa NFF Amaju Pinnick amesema kuwa wamekubaliana.

Keshi ambaye amehudumu katika wadhfa huo tangu mwaka wa 2011 amepewa kandarasi mpya ya miaka miwili.
Keshi anakumbukwa kwa ushindi wa kombe la mataifa ya Afrika katika awamu yake ya kwanza mwaka wa 2013.
''Sote kama kamati tumekaa na kukubaliana kuwa Keshi anastahili kuendelea na majukumu yake katika timu ya taifa''
''Naamina kuwa ataweka sahihi karibuni na kuanza kazi'' alisema Pinnick.

Hata hivyo LEKULE BLOG inaamini kuwa Keshi amewekewa malengo maalum ambayo asipoyataimizwa makubaliano yao huenda yakatibuka.
Hivi sasa Keshi anakabiliana na upinzani mkubwa Nigeria, baada ya The Cranes kuiangusha The Super Eagles 1-0 hapo jana.
Aidha Keshi alishindwa kuisaidia Nigeria kwenye kombe la mataifa Afrika ilioandaliwa huko Equatorial Guinea.

No comments: