Jopo laundwa kuchunguza viongozi Kenya - LEKULE

Breaking

31 Mar 2015

Jopo laundwa kuchunguza viongozi Kenya



Jopo maalum limeundwa ilikuwachunguza maafisa wakuu serikalini na wanasiasa ambao wametuhumiwa kuhusika na ufusadi.

Idara ya kuchunguza masuala ya jinai,tume ya kukabiliana na ufisadi pamoja na afisi ya mashtaka ya umma zinasema zimekamilisha baadhi ya kesi.

Mashirika ya kiraia yamekua yakimshinikiza rais Uhuru Kenyatta kuwataja wote wanaotuhimiwa na ufisadi ambao umesababishia nchi kupoteza mamilioni ya pesa.

Waziri wa kilimo wa Kenya akiandamana na mawakili kadhaa, aliwasilia katika makao makuu ya tume ya kupambana na ufisadi,

muda mfupi baada ya saa sita za mchana majira ya Afrika Mashariki, huku akiwa kwenye msafara wa magari matatu ya kifahari.

Akiwa amevalia suti ya kijivu, waziri huyo alionekana mchangamfu kinyume na unavyomtarajia kiongozi aliyesimamisha kazi.

Kabla ya kuingia ndani aliwafahamisha waandishi wa habari kuwa hana lolote hadi atakapomaliza.

Dakika arubaini na tano baadaye, Kosgei alijitokeza tena na kusema kuwa ameshauriana na mmoja wa wakurugenzi wa tume hiyo, na kinyume na alivyotarajia,

alifahamishwa kuwa kwa sasa tume hiyo haina nyaraka zozote za kuonyesha sababu zilizopelekea jina lake kuorodheshwa miongoni mwa washukiwa wa ufisadi. Kupitia kwa mawakili wake Kosgei alikuwa ametaka tume hiyo kumweleza madai dhidi yake,

orodha ya walalamishi, nyaraka zilizowasilishwa mbele ya tume hiyo na walalamishi au stakabadhi zozote kuhusiana na madai yanayomkabili.

Waziri huyo aliyesimamisha kazi itabidi asuburi hadi siku ya alhamisi wiki hii.

Mawaziri watano na maafisa wengine wengi wa taasisi za umma wamesimamishwa kazi kwa muda kuhusiana na madai ya kuhusika na ufisadi.

Akilihutubia bunge la Kenya wiki iliyopita, rais Uhuru Kenyatta aliagiza maafisa wote wakuu serikalini waliotajwa na tume ya kupambana na ufisadi

kungatuka madarakani kwa muda wa siku sitini ili kuruhusu uchunguzi wa kina.

Kwingineko, jopo maalum limeundwa ili kuchunguza madai dhidi ya mawaziri hao na maafisa wakuu serikaini,

ambo wamesimamishwa kazi nchini Kenya kuambatana na agizo la rais Kenyatta, kuwa maafisa hao wana siku sitini kukamilisha uchunguzi huo

Jopo hilo litajumuisha maafisa kutoka idara ya mashtaka ya umma, tume ya kupambana na ufisadi na idara ya ujasusi.

Wakati huo huo maafisa wa kaunti ya nairobi leo walinasa punda watano waliokuwa wamefungwa na minyororo kati kati mwa mji mkuu.

Punda hao walikuwa wamepakwa rangi nyekundu na maandishi yanayopinga ufisadi.

Punda mmoja alikuwa na maandishi ya kimombo ''Corruption bleeding Kenya dry'' yaani Ufisadi unamaliza taifa la Kenya

Punda mwingine naye alikuwa na maandishi mengine mgongoni inayowakejeli baadhi ya wabunge wa Kenya ambao wametuhumiwa kuhusika na unyanyazaji wa kimapenzi.

No comments: