Huduma ya Texi yasitishwa Ujerumani - LEKULE

Breaking

22 Mar 2015

Huduma ya Texi yasitishwa Ujerumani

Ni wiki ngumu ya Uber.Mahakama moja nchini Ujerumani imepiga marufuku huduma ya bei nafuu ya texi ya Uberpop baada ya kuamua kwamba inaenda kinyume na sheria za uchukuzi.Vilevile afisi za kampuni hiyo zilizopo mjini Paris zimevamiwa na maafisa wa polisi wa Ufaransa wanaochunguza huduma hiyo ya Uberpop,huku watu 30 wanaohusishwa na kampuni hiyo wakishtakiwa kwa kuendesha kampuni hiyo ya texi nchini Korea Kusini bila vibali.Uber imesema kuwa wafanyikazi wake wa koreakusini hawajavunja sheria na kuutaja uvamizi huo wa Paris kama usio wa haki.

No comments: