Hatimaye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha miswada miwili iliyowekwa kiporo kutoka katika mikutano iliyopita ya Bunge kwa sababu tofauti.
Miswada hiyo ni Muswada wa Sheria ya Takwimu na Muswada wa Usamizi wa kodi ya mwaka 2014, ambayo haikuweza kupita kutokana na kukosa akidi na pamoja na kuhitaji kufanyiwa marekebisho.
Mswada wa sheria ya Takwimu haukuweza kupitishwa baada ya kusomwa mara ya pili kutokana na wabunge wengi kupinga na kutaka kufanyiwa marekebisho baadhi ya vifungu huku ule wa usimazi wa kodi ukikosa akidi katika kupitishwa kwake.
Licha ya kupitishwa kwa Muswada ya Sheria ya Takwimu, mbunge John Mnyika kwa niaba ya Ezekiel Wenje ameonesha kupinga baadhi ya vifungu hususani vinavyohusu adhabu kwa vyombo vya habari vinavyotoa takwimu zisizosahihi.
Awali kabla ya Miswada hiyo kupitishwa, Bunge limejadili na kupitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Uhamiaji wa Mwaka 2014.

No comments:
Post a Comment