Boko Haram kuiga mfano wa Islamic State - LEKULE

Breaking

8 Mar 2015

Boko Haram kuiga mfano wa Islamic State



Kiongozi wa kundi la wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria ametoa taarifa akiahidi kuliheshimu kundi la wapiganaji wa Islamic state.

Abubakr Shekau alitoa tangazo hilo katika ujumbe wa sauti uliowekwa katika mtandao,ambapo aliwaagiza waislamu wengine kuiga mfano wake.



Haijulikani ni vipi muungano huo utakuwa lakini mwandishi wa BBC katika eneo la mashariki ya kati anasema ni propaganda za kundi la Islamic State ambalo limekuwa likishindwa katika makabiliano nchini Iraq na Syria.

Kundi la wapiganaji wa Boko Haram limetekeleza mashambulizi kadhaa kwa lengo la kutaka kuweka utawala wa kiislamu kazkazini mwa Nigeria ambapo maelfu ya watu wameuawa.

No comments: