Askari na Waasi wauawa kwa Bomu Syria - LEKULE

Breaking

5 Mar 2015

Askari na Waasi wauawa kwa Bomu Syria

Waasi nchini Syria na askari wa usalama wameripotiwa kuuawa katika mapigano katika mji ulio kaskazini mwa Nchi hiyo, Aleppo.
Mapigano yalianza kwa kusikika milipuko iliyolenga Makao makuu ya ya kikosi cha upelelezi cha jeshi la anga nchini Syria.
Inakisiwa kuwa Waasi walijipenyeza chini ya Jengo hilo ili kutega bomu, kisha baadae mlipuko ulisikika na mapigano yanaendelea.
Wanamgambo wanaotii kundi la kiislam la Nusra Front lenye uhusiano na Al Qaeda wamekiri kutekeleza shambulio hilo.
Makundi kadhaa ya Waasi yamekuwa yakipambana na Vikosi vya Serikali ili kuudhibiti Mji wa Aleppo kwa kipindi cha miaka miwili na nusu licha ya jitihada za Umoja wa Mataifa kumaliza mzozo.

No comments: