Jeshi la polisi mkoani Simiyu linawashikilia askari wawili wa jeshi la
magereza na polisi kwa kukutwa na noti bandia ikiwa ni pamoja na sare za
jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ).
Akitoa taarifa za kukamatwa
kwa askari hao, Kamanda wa polisi mkoani hapa Naibu Kamishina, Charles
Mkumbo alisema kuwa askari hao walikamatwa juzi majira ya saa 9 mchana
katika mtaa wa Old Maswa kata ya Nyakabindi Wilayani Bariadi.
Mkumbo
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni askari mwenye namba H 2420 PC Seleman
Juma (25) ambaye ni askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) Mkoani
Simiyu, na askari namba B.6499 WDR Edmund Masaga (28) ambaye ni askari
Magereza wilayani Bariadi.
Kamanda Mkumbo alieleza kuwa baada ya
askari hao kukamatwa mmoja wao PC Selemani Juma alipopekuliwa katika
mfuko wa suruali yake alikutwa na noti zingine za Bandia za elfu kumi
kumi na jumla yake kama zingelikuwa halali zingelikuwa na thamani ya
Shilingi 1,920,000.
Alisema kuwa askari hao walifika kwenye
kibanda cha M-pesa kinachomilikiwa na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Old
Maswa, Kassian Luhende (29) wakiwa na pikipiki yenye namba za usajili T
403 CXW aina ya Sunlg kwa lengo la kuweka fedha hizo kwenye simu.
Baadhi ya noti bandia walizokutwa nazo
No comments:
Post a Comment