WAYAHUDI NA WAISLAMU WAUNGANA NORWAY - LEKULE

Breaking

22 Feb 2015

WAYAHUDI NA WAISLAMU WAUNGANA NORWAY


Waislamu nchini Norway wakiweka mviringo wa kuwazunguka wayahudi ili kuonyesha amani kufuatia misururu ya mashambulizi inaowalenga raia hao.
Zaidi ya watu 1000 wengi wao wakiwa waislamu wameunda mviringo na kulizunguka sinagogi nchini Norway kuonyesha umoja wao kufuatia mashambulizi kadha yaliyowalenga wayahudi barani Ulaya.
Wakati waumini wa kiyahudi walipokuwa wakitoka ndani ya sinagogi katika mji mkuu wa Norway Oslo kulikuwa na shangwe wakati vijana wa kiislamu walipowazingira kama ishara ya amani.
Warsha hiyo ilipangwa na vijana wa kiislamu na inafanyika wiki chache baada ya kijana mmoja mzaliwa wa Denmark mwenye asili ya Kipalestina kuwaua watu wawili.

No comments: