Wasichana watorokea Syria kujiunga na IS - LEKULE

Breaking

22 Feb 2015

Wasichana watorokea Syria kujiunga na IS

 Familia za wasichana watatu raia wa Uingereza ambao wanakisiwa kusafiri kwenda nchini Syria kujiunga na kundi la Islamic State zimewasihi kurudi nyumbani.
Wasichana hao kutoka mji mkuu wa Uingereza London walionekana mara ya mwisho walipopanda ndege iliyokuwa ikienda nchini Uturuki.
Familia ya msichana mmoja mwenye umri wa miaka 15 ilisema kuwa inaelewa kuwa alikuwa na nia ya kuwasaidia wale wanao taabika nchini Syria lakini eneo hilo ni hatari.
Nayo familia ya mwanamke mwingine raia wa Uingereza ambaye anashukiwa kupanga safari za wasichana hao baada ya kusafiri kwenda nchini Syria mwaka 2013 imelaani vitendo vyake.

No comments: