Ebola:Liberia sasa yafungua mipaka yake - LEKULE

Breaking

22 Feb 2015

Ebola:Liberia sasa yafungua mipaka yake


 Mipaka ya Liberia imefunguliwa rasmi, miezi 7 baada ya kufungwa kwa sababu ya janga la ebola.

Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, alisema hatua zitachukuliwa kuhakikisha kuwa virusi vya Ebola havitoingia tena nchini kwa kupitia mpakani.

Amri ya kutotoka nje usiku itaondoshwa leo.

Idadi ya watu wanaoambukizwa Ebola nchini Liberia, ni asilimia 10 tu na ilivyokuwa wakati wa kilele cha ugonjwa huo.

No comments: