Mahakama ya Misri imeunga mkono hukumu ya kifo dhidi ya wanachama 183 wa Muslim Brotherhood kufuatia shambulizi moja la kituo cha polisi mwaka 2013 karibu na Cairo.
Wanachama hao walishtakiwa kwa kuwaua maafisa 11 wa polisi.
Shambulizi hilo lilitekelezwa baada ya jeshi la Misri kukabiliana na waandamanaji waliomng'oa mamlakani rais Mohammed Morsi mnamo mwezi Julai.
Zaidi ya hukumu 100 za kifo zimetolewa dhidi ya wafuasi wa Morsi lakini hakuna hata moja iliotekelezwa.
No comments:
Post a Comment