Wananchi wenye hasira mjini Ilula, mkoani Iringa, wamevamia kituo cha polisi na kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, tukio hilo limetokea leo kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina lake wakati anakimbia alichotwa mtama na Polisi na kusababisha mama wa watu kuanguka na kufariki hapo hapo .
Mama huyo alikuwa anawakimbia polisi waliokuwa kwenye oparesheni ya kuwakamata watu wanaokunywa pombe wakati wa asubuhi.
Habari zaidi zinapasha kwamba, licha ya kuchoma moto magari, waliziba barabara kuu ya kwenda mikoani na kuyazuia magari kupita, hali iliyosababisha polisi kuwakabili lakini walizidiwa nguvu na kuingia ndani ya basi la Nyagawa.
Askari wakiwa ndani ya gari hilo waliendelea kushambuliwa na wananchi kwa mawe na kuvunja vioo vyake.
No comments:
Post a Comment