IS yawateka wakristu 90 Syria - LEKULE

Breaking

24 Feb 2015

IS yawateka wakristu 90 Syria

Kundi la Islamic State limewateka nyara watu 90 wa jamii ya wakristo kutoka katika kijiji kimoja kazkazini mwa Syria.

Kisa hicho cha utekaji nyara kilifanyika mapema leo alfajiri, baada ya wanamgambo hao kuchukua udhibiti wa vijiji kadhaa kutoka kwa walinda usalama wa kabila la Wakurdi.

Wanamgambo hao walivamia kituo cha Radio na kuchukua udhibiti wa mawasiliano na kuanza kutangaza Radioni, kuwa wamewateka nyara wale wanaojiita watetezi wa Dini.

Kwa muda mrefu kundi la wakristo wachache walioko Nchini humo limekuwa likishirikiana na wapiganaji wa kabila la Wakurdi kukabiliana na wanamgambo wa IS.
Awali Kundi la I S limekuwa likiharibu makanisa ya wakristo Nchini Syria.

Wakristo hao wa makabila ya Assyria ambao wengi wamo serikalini, wanaiunga mkono utawala wa sasa wa Syria na wamekuwa wakipigana na wanamgambo hao wa Islamic State.

Idadi ya Wakristo katika maeneo hayo imepungua kwa kasi mno kutokana na mauwaji dhidi yao.

No comments: