Kilabu ya Manchester United
inasubiri kujua ubaya wa jeraha la mshambuliaji wake Robin Van Persie
baada ya mchezaji huyo kuondoka katika uwanja wa Liberty akitumia
magongo.
Van Persie mwenye umri wa miaka 31 pia alionekana
amefungwa mbamba katika mguu wake wa kulia baada ya kupata jeraha katika
mda wa lala salama wa mechi dhidi ya Swansea ambapo Swansea waliibuka
kidedea jumamosi.Msimu huu Robin Van Persie ameifungia Manchester United mabao 10,lakini hakuweza kutolewa kwa kuwa United tayari ilikuwa imefanya mabadiliko matatu.
No comments:
Post a Comment