Kilabu ya Manchester City ilipata
ushindi wao mkubwa zaidi katika ligi ya EPL msimu huu kwa kuicharaza
Newcastle 5-0 na hivyobasi kupunguza pengo lililopo kati yake na
viongozi wa ligi kwa sasa Chelsea hadi pointi tano.
David Silva alifunga mabao mawili katika ushindi mkubwa baada ya kilabu ya Burnley kupata sare ya 1-1 dhidi ya Chelsea.Huku Yaya Toure akiwa amerudi kutoka dimba la mataifa ya Afrika naye Wilfried Bonny akiwa ameanza kama mchezaji wa Ziada,City ilianza mechi hiyo kwa kasi ikilinganishwa na mechi zao nyingine katika uwanja wa nyumbani Etihad.
Mancity ilifunga mabao yake kupitia Aguerro,Dzeko na Samir Nasri.
No comments:
Post a Comment