Pato la Taifa kwa kipindi cha Robo ya Tatu ya Mwaka 2014 toka Julai mpaka hadi Septemba 2014 limekuwa na kufikia Trillion 21.2 ikilinganishwa na Trillion 19.8 kipindi kama hiki mwaka 2013.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi toka Ofisi ya Taifa za Takwimu Mourice Oyuke alisema kuwa kukuwa kwa pato la taifa kumetokana na kuongezeka kwa uzalishaji katika robo ya tatu ya mwaka 2013.
Pamoja na ukuaji huo wa Pato la Taifa kwa Robo mwaka lakini kasi ya kukua kwa uchumi imepungua toka Asilimia 7.4 mwaka 2014 hadi Asilimia 6.8 mwaka 2015 kutokana na kupungua kwa shughuli za kilimo na uzalishaji viwandani
No comments:
Post a Comment