Qatar yamuondoa Balozi wake Misri - LEKULE

Breaking

19 Feb 2015

Qatar yamuondoa Balozi wake Misri







Vyombo vya habari nchini Qatar vimesema Serikali ya nchi hiyo vimemuondoa Balozi wake nchini Misri.
Ripoti zinasema kuwa hatua ya kumuondoa Balozi wake imekuja baada ya Kauli ya mwakilishi wa Misri kwenye jumuia ya nchi za kiarabu kutoa matamshi yanayoashiria kuwa Qatar imekuwa ikiwaunga mkono wanamgambo wa kiislamu nchini Libya.
Matamshi hayo yamekuja baada ya Misri kufanya mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Jihad nchini Libya wakilipa kisasi kuhusu tukio la wakristo wa kikopti kuuawa na kundi la IS.

No comments: