Serikali ya Libya inayotambuliwa
kimataifa imeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiondolea
nchi hiyo vikwazo vya silaha ili kukabiliana na kuzorota kwa hali ya
usalama nchini humo.
Akihutubia kikao cha dharura cha baraza hilo,
waziri wa mambo ya nje wa Libya,Mohammed al-Dairi amesema hatua hiyo
itaisaidia serikali ya Libya kujenga jeshi lake, ili kuwatokomeza
Islamic State na makundi mengine ya wapiganaji.Waziri huyo wa mambo ya nje wa Libya aliungwa mkono na waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry, ambaye amesema jumuia ya kimataifa inatakiwa kuisaidia serikali ya Libya ili kuonyesha mamlaka yake nchini humo.
Mapema wiki hii, ilithibitika kuwa wapiganaji wa Islamic State nchini Libya waliwakata vichwa mateka kutoka Misri.
No comments:
Post a Comment