Mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarab nchini ambaye pia ni mkurugenzi
wa kundi la Jahazi Modern Taarabu,Mzee Yusuph anatarajia kuoa tena mke
wa tatu hivi karibuni huku wake zake wawili wakiwa kwenye bifu zito
wakitupiana vijembe mtandaoni.
Akipiga stori na Uheard na Soudy Brown alisema kuwa anatarajia kuoa
mke huyo ambaye anaishi huko visiwani Pemba,na kwamba mipango ikiwa
tayari kila kitu kitakuwa hadharani.
Hivi karibuni wake zake wawili ambao ni Malkia Leila Rashid ambaye
pia ni mwimbaji wa kundi hilo na mke wake mdogo aitwaye Chiku wamekuwa
wakirushiana vijembe kwenye mtandao wa kijamii wa ‘WathsAAp’ kwa
kuandikiana ‘Status’ za vijembe.
Habari zinasema kuwa wake hao wamekuwa kama chui na paka na mzee
Yusuph hana mpango wa kuwapatanisha kwa kuwa hakuna hata mmoja
aliyeonyesha chuki kwa mwenzake akiwa na nao.
Waache tu warushiane vijembe tena ndiyo vizuri na dawa yao nawaletea
mke wa tatu na wala sina mpango wa kuwapatanisha,"alisema Mzee Yusuph.
No comments:
Post a Comment