Mwigizaji
mkongwe wa vichekesho hapa Bongo, Rashid Mwinshehe "Kingwendu", amesema
anajiandaa Kugombea Ubunge 2015 Kupitia Chama ambacho amedai Kuwa
anaona Kinapendwa na Watanzania wengi bila ya Kutaja Jina la Chama hicho
wala Jimbo atakalogombea.
Wataalamu
wa Masuala ya Kisiasa Nchini, wameitafsiri Kauli hiyo ya Kingwendu Kwa
Mitazamo tofauti, huku Wengi Kati yao Wakisema Kuwa Upinzani Una Nguvu
Kubwa hivi sasa hapa Nchini, hivyo Sio ajabu Kwamba yawezekana Msanii
huyu amevutiwa na Kuamua Kujiunga na Chama fulani Cha Upinzani Ili
aendeshe harakati za Ukombozi wa Taifa hili.
Akizungumza na Mwandishi wa Tanzania Daima, Kingwendu alisema,
"Ninajiandaa Kugombea Ubunge 2015 Kupitia Chama ninachoona Kinapendwa
na Watanzania wengi Kwenye Jimbo ambalo ntalitaja hapo baadae Wakati
Utakapofika...
"Bado ninafanya Mazungumzo na Washauri wangu wa Karibu Kuhusiana na Swala, nadhani ntaliweka Wazi muda Ukifika..."
No comments:
Post a Comment