Maduka ya wafanyabiashara mbalimbali yaliyopo mtaa wa India jijini Tanga yameteketea kwa moto kwa kile kinachodaiwa kuwa imetokana na hitilafu ya umeme.
Moto huo uliokuwa ukifukuta ndani katika maeneo hayo ya biashara ulisababisha baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo kutaka kulishambulia gari la zima moto la halmshauri ya jiji la Tanga kufuatia kufika katika eneo la tukio lakini wakati linaaza zoezi hilo ghafla likaishiwa maji katika kipindi cha dakika 3 na kuamsha hasira kwa mamia ya wananchi.
Hata hivyo akielezea hatua hiyo kamanda wa opesheni wa kikosi cha zima moto mkoani Tanga Bwana Kumenya Bakari amekemea vikali jazba za wananchi za kushambulia mara kwa mara gari la zima moto la halmashauri ya jiji la Tanga na kufafanua kuwa wanapofika katika eneo la tukio jambo la kwanza wanaanza kwanza kuokoa maisha ya watu, mali ndio kisha baadaye kuzima moto katika eneo husika.
No comments:
Post a Comment