Misri si mwenyeji wa AFCON 2017 - LEKULE

Breaking

24 Feb 2015

Misri si mwenyeji wa AFCON 2017

waziri wa michezo nchini Egypt Khaled Abdel-Aziz amethibitisha kuwa nchi yake imetupilia mbali jitihada zake za kuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2017.

Anasema,tumeamua kujiondoa kwenye maombi hayo na tutawaunga mkono Algeria.

Nchi za Gabon na Ghana ziliomba zabuni hiyo ,nalo shirikisho la soka barani Africa litatoa jina la mwenyeji wa michuano hiyo mnamo tarehe 8 ya mwezi April.

Libya nayo ilikuwa na tamanio la kuwa mwenyeji wa fainali za michuano hiyo lakini ilijiondoa kutokana na hali ya kisiasa inayoendelea nchini humo.

Waziri Abdel-Aziz hakufunguka zaidi kueleza sababu za ziada za kujiondoa lakini imeshikilia msimamo huo baada ya mjumbe wa kamati ya utendaji ya FIFA ,Hany Abu Rida kusema kwamba haina maana yoyote kwa nchi mbili za kiarabu kushindania zabunia hiyo.

Anasema Egypt haitaweza kushindana na Algeria lakini tuna hakikisha kutoa usaidizi makini kadiri tuwezavyo anahakikisha Abu Rida katika maelezo yake.

Kujiondoa huko kunakuja baada ya vifo vya mashabiki 22 mnamo tarehe 8 February wakati polisi na washabiki walipovaana kabla ya mchezo baina ya timu ya Zamalek ya Cairo na ENPPI.

Kufuatia tukio hilo shughuli zote za soka za ndani zimesimamishwa mpaka hapo itakapotangazwa tena lakini waziri mkuu wa Misri Ibrahim Mahlab anaamini kuwa ligi ya nchi hiyo haitaishia kufutwa ingawa kwa sasa tunaangalia zaidi suala la usalama michezoni na kupisha hali mbaya ya hewa iliyotokea michezoni.

Waziri huyo ametoa ahadi ya kujadili suala hilo wiki ijayo na kutilia mkazo vipaumbele vya mazungumzo hayo kuwa ni kuweka mambo katika mizania na hasa ligi kurejeshwa tena na suala la usalama wa wanamichezo.

Na kama Ligi itaendelea basi washabiki hawatahitajika uwanjani Mahlab ameelezea msimamo wa nchi yake.

Tukio hilo la hivi karibuni lililotokea katika mzunguuko wa kwanza wa ligi nchini humo,ambalo linakuja na amri ya kutoruhusu mashabiki uwanjani ili kunusuru usalama mchezoni,ikumbukwe kwamba tangu February mwaka 2012 mashabiki walipigwa marufuku kushuhudia mechi zikipigwa uwanjani kutokana na washabiki takribani sabini na wawili wa Al Ahly walipovaana na mashabiki wa timu ya Al Masry katika uwanja wa Port Said na kusababisha maafa hayo.

No comments: