Fainali za kombe la dunia kwa mwaka 2022 nchini Qatar huenda sasa zitafanyika mwezi Novemba au Decemba hiyo ni kwa mujibu wa Mkuu wa kikosi kazi cha shirikisho la kandanda duniani Sheikh Salman Bin Ebrahim amesema mapendekezo ilikuwa iwe mwezi May lakini wakati huo utakuwa vigumu kwani ni majira ya fainali za michuano fainali za Klabu Bingwa barani Ulaya.
Nchi ya Qatar imepewa jukumu la kuandaa mashindano hayo mwaka 2022 lakini imegundulika kuwa fainali hizo zitagongana na majira ya joto kali katika eneo hilo, jambo ambalo ni kikwazo wa afya za wachezaji.
Mapendekezo mengine yalikuwa iwe kati ya mwezi Januari au Februari lakini imeonekana zitagongana na mashindano ya Olympic.
Hassan Al Thawad mkuu wa kamati ya maandalizi ya finali hizo nchini Qatar ameiambia BBC kuwa Qatar imekubaliana na mapendekezo ya kamati ya shirikisho la kanda nda duniani Fifa.

No comments:
Post a Comment