Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe
ametangaza mpango maalumu wa wapenzi na wanachama wa chama hicho
kuchangia Sh10,000 kwa mwezi ili kupata fedha za kutosha kukiendesha
chama ikwa lengo la kuiondoa CCM madarakani kupitia Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) kwa njia ya kura.
Mbowe alitoa kauli
hiyo juzi wakati akihutubia mamia ya wakazi na wafuasi wa chama hicho
katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini
Mbeya.
Akifafanua kuhusu michango hiyo kwa kutumia
mfano alisema, kama eneo la Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini watapatikana
watu milioni moja watakuwa wamechanga kwa mwezi Sh100 milioni ambazo
zinatosha kuing’oa CCM katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.
Mbowe
alisema, Chadema imefanikiwa kuiteka mikoa yote muhimu katika nchi
ambayo ipo vizuri kiuchumi na kukubaliwa na wananchi, hivyo njia ni
nyeupe kwa upinzani kuingia Ikulu.
Mbowe alisema
kutokana na fursa hiyo Chadema kukubaliwa na taifa hili na CCM kupoteza
mwelekeo ndiyo sababu ya wao kushinda uchaguzi.
Awali,
Naibu Katibu Mkuu Chadema (Zanzibar), Salumu Mwalimu alisema upinzani
umejipanga vilivyo na umedhamiria kuingia Ikulu mwaka huu huku
akibainisha kwamba mara baada ya kuingia Ikulu jambo la kwanza ni
kuwarudishia Watanzania Katiba yao waliyoipendekeza na siyo vinginevyo.
Wabunge
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ wa Mbeya Mjini na Mchungaji Peter Msigwa wa
Iringa Mjini, walisema hali ya kisiasa kwa upande wa Chadema katika
ukanda wa Nyanda za Juu Kusini umeimairika hivyo kazi iliyopo ni kupata
wagombea wenye sifa ya kukubalika na wananchi, muda uliobakia watafanya
kazi ya kuzunguka mikoa yote ya ukanda huo.
No comments:
Post a Comment