Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF)
Profesa Ibrahim Lipumba leo amewasihi Jumuiya ya Vijana wa CUF(JUVICUF)
kusitisha maandamano kama jeshi la polisi lilivyoagiza .
Akizungumza leo katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni, jijini
Dar e s Salaam, amesema kuwa vijana hao waache kuandamana kwa sababu
kunaweza kutokea madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kupigwa risasi,
vifo na kadhalika.
Alisisitiza waache kuandamana ingawa dhamira yao ya kuitaka Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC) iongeze siku za uandikishwaji wa upigaji kura
kutoka siku saba hadi 14 ina mantiki kwa Watanzania wote.
JIVICUF
walikuwa waandamane kusisitiza, miongoni mwa mambo mengine, kuhusu
uvunjwaji wa haki za binadamu nchini na dosari za uandikishaji wapiga
kura.
No comments:
Post a Comment