Haya ni maoni ya mwanasheria kijana, Alberto Msando kuhusu makosa ya
uandishi wa lugha ya kingereza kwenye kasha la filamu ya Mzee wa Swaga,
iliyotengenezwa na kampuni ya Jerusalem, inayomilikiwa na msanii nguli
wa filamu, Jacob Stephen 'JB '.
Alberto aliandika haya mara baada ya kubandika picha hiyo ya kwenye kasha :
“Bado ni marafiki zangu tu. Ninachotaka ni sanaa yenu ipendwe na
watanzania waithamini. Soko la ndani ni kubwa sana. Ila endapo tu
mtazingatia ubora.
"Najua mtaji wa kuwekeza kwenye filamu ni kazi
kuupata. Basi hayo makubwa tuyaache. Tubaki na haya madogo ambayo yako
ndani ya uwezo wenu.
"Hakuna from produced of shikamoo mzee. Na hakuna
enterianments. Kiswahili ni sawa pia kutumia. Kwani ingeandikwa
'Imeandaliwa na' kuna shida?
"Na hakuna auto correct ya entertainment?
UTASIKIA utetezi wa kitoto; sio lugha yetu!! Au ni bahati
mbaya!”-Alberto alimalizia
No comments:
Post a Comment