Kocha:Ronaldo kung'ara dhidi ya Schalke - LEKULE

Breaking

18 Feb 2015

Kocha:Ronaldo kung'ara dhidi ya Schalke



Mkufunzi wa kilabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti anaamini mchezaji nyota Christiano Ronaldo ataimarika punde tu atakapopata bao.

Mchezaji huyo wa Ureno hajafunga katika mechi zake tatu zilizopita ,na hivyobasi kuzua utata kuhusu kiwango cha mchezo wake kabla ya mechi ya kilabu bingwa Ulaya dhidi ya Schalke.

Ronaldo amekuwa akiugua jeraha la mguu,lakini kocha Ancelotti hana wasiwasi.

''Itakuwa fursa kwa yeye kupata bao wakati wa mechi dhidi ya Schalke'',alisema.

Ni kipindi cha mda mrefu kwa Ronaldo kucheza bila kufunga msimu huu licha ya yeye kupata mabao 38 katika mechi 35.

No comments: