Wakazi
wa kijiji cha Uchindile wilayani Ifakara mkoani Morogoro wamepata
umeme unaozalishwa kwa kutumia kuni baada ya kuzinduliwa kwa mtambo wa
10kW uliotolewa na kampuni ya kimataifa ya Camco Clean Energy.
Mtambo
huo wenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 75 ulizinduliwa na Mwakilishi
wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID), Rogness Swai katika hafla
iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta hiyo, wakiwemo wananchi wa
kijiji hicho.
Pamoja
na Camco Clean Energy Tanzania iliyofadhiliwa na USAID ili kufanikisha
mradi huo utakaokabidhiwa kwa serikali ya kijiji hicho, Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni hiyo nchini, Jeff Felten aliwataja wengine
waliochangia ujenzi wake kuwa ni kampuni ya Village Industrial Power
(VIP) na Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi (MPM) cha Mgololo, wilayani
Mufindi.
Felten
alisema mtambo huo utawezesha kaya 100 kati ya 265 za kijiji hicho
kilichopo zaidi ya kilomita 100 toka Mafinga, wilayani Mufindi mkoani
Iringa kuwa za kwanza nchini kunufaika na nishati hiyo inayotarajiwa pia
kuzinduliwa mkoani Kigoma hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment