Matokeo ya upangwaji wa droo ya timu
16 ya ligi ya Europa zitafanyika leo nchini Uswisi kuanzia saa tisa kwa
saa za Afrika Mashariki.
Droo hiyo itasimamiwa na Katibu Mkuu wa
UEFA, Gianni Infantino, na Mkurugenzi wa Mashindano wa UEFA, Giorgio
Marchetti, pamoja na Jerzy Dudek, Kipa wa zamani wa timu ya taifa ya
Poland, ambae ndiye Balozi wa fainali ya Mwaka huu ya Europa Ligi
itakayochezwa huko Poland, Mei 27.Droo hii itahusisha timu 16 zilizofuzu toka kwenye timu 32 ambapo jana usiku zilikamilisha michezo yao ya marudiano.
Michezo ya mtoano itapigwa kuanzia Machi 12 na Marudiano Machi 19 na Washindi kutinga hatua ya Robo fainali.
No comments:
Post a Comment