BONDIA IDDI BONGE KUZIPIGA LEO NA ALFONCE MCHUMIATUMBO TPA SABASABA - LEKULE

Breaking

14 Feb 2015

BONDIA IDDI BONGE KUZIPIGA LEO NA ALFONCE MCHUMIATUMBO TPA SABASABA

Bondia Iddi Bonge akipiga beg zito wakati wa mazoezi yake ya mpambano wake na Aliphoce Mchumiatumbo utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba siku ya feb 14 


Bondia Iddi Bonge akipiga beg zito wakati wa mazoezi yake ya mpambano wake na Aliphoce Mchumiatumbo utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba siku ya feb 14 

BONDIA IDDY BONGE AKIWA NA MARAFIKI ZAKE ANAOFANYA NAO MAZOEZI 


Bondia Iddi Kipandu 'Iddi Bonge ' amendelea na mazoezi kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika feb 14 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba ambapo atapambana na Alphonce Mchemiatumbo  mpambano wa ubingwa wa taifa raundi kumi uzito wa juu ni kwa mara ya kwanza kabisa baada ya miaka kadhaa kupita na kuto kuwa na bingwa wa uzito wa juu

akizungumza wakati wa mazoezi yake anayofanya katika gym ya garden iliyopo mburahati jijini Dar es salaam amesema yeye amejipanga kwa raundi kumi lakini ata hivyo azitoisha kutokana na ngumi zake kuwa nzito zana na anatarajia kumaliza mpambano mapema hivyo mashabiki wawai mapema kuja kuangalia mpambano wao uho uliovuta hisia kali za mashabiki wa Temeke na Kinondoni

nae mratibu wa mpambano huo wa uzito wa juu Shabani Manyoka amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na wanasubili siku ya mpambano tu ata hivyo ijumaa watapima uzito katika ofisi za chama cha ngumi za kulipwa nchini kinachongozwa na Emanuel Mlundwa ofisi zilizopo DDC Keko Dar es salaam


mpambano huo wa raundi kumi utakuwa ni wa aina yake kwa kuwa kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambapo bondia Iddi Mnyeke atapambana na Yonas Sego nae Antony Mathias atakabiliana na bondia chipkizi anaekuja kwa kasi katika ulimwengu wa masumbwi Vicent Mbilinyi wakati Shabani Kaoneka atamkabili Saidi Mbelwa, na Deo Samweli akipambana na Adam Ngange Juma fundi atakabiliana na Bakari Ostadhi na Amani Bariki 'Manny Chuga' atapambana na Mohamed Kashinde 
 

Manyoka aliongeza kwa kusema kuwa siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha ndani na nje ya ukumbi huo ambapo amesha wasiliana na walinzi mbalimbali
siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali 
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo




No comments: