Bond asikitishwa na tuhuma za kuwa na watoto wanne na kumsababishia Wastara kuzimia - LEKULE

Breaking

27 Feb 2015

Bond asikitishwa na tuhuma za kuwa na watoto wanne na kumsababishia Wastara kuzimia


Mtangazaji, Mwigizaji na muongozaji wa filamu Bond Bin Sinnan ambae pia ni meneja wa mwigizaji Wastara Juma amejitoteza mtandaoni na kuonesha kupinga kile ambacho kilandikwa na magezi ya udaku kuwa ana watoto  watatuna na mmoja  amezaliwa majuzi  na baada ya Wastara kupigiwa simu mpenzi wazamani wa Bond, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ kujulishwa kuwa “demu” wa Bond amezaa na inadaiwa Wastara alizimia baada ya kusikia taarifa hizo.

Sasa jana Bond ameibuka na kubandika haya mtandaoni.

"Binadamu wengine bana wanadhani ustar unakuja kwa kuandikwa kwenye magazeti tu.
Yaani mtu anakosa kazi ya kumfanya aandikwe magazetini basi anaona andikwe kupitia watu.. eti unawafata watu wa magazeti na kuanza kusema uongo kisa uonekane unanijua sana.. dah eti nina watoto wanne? We unawajua? Mama zao wataje basi, na magazeti mengine uchwala kweli ati mtu anakuja kuwaambia muandike kitu nanyi mnaandika..ntakuja kuwaambia mjiandike na nyinyi..huna ushahidi wowote na jambo unaandika kweli? 
Ila ipo siku yenu mtafurahi tu in shaa allah...kila jambo linakuja kwa sababu.. alhamdulillah..."- Bond alimaliza.

Hadi sasa Wastara  ajazungumzia chochote kuhusu tuhuma hizi, labda akatuwa ameamua kuzipuuzia bila shaka!.

No comments: