Kiungo wa timu ya taifa ya Ivory Coast ambaye pia ni nahodha wa timu
hiyo Yaya Toure hapo jana alizua hofu kwa mashabiki wa timu hiyo baada
ya kulazimika kukosa mazoezi ya timu hiyo baada ya kupata jeraha .
Toure alilazimika kukatisha mazoezi yake na kukaa nje akiugulia kwa maumivu huku madaktari wa timu hiyo wakimtibia taswira ambayo ilizua hofu kubwa ya kiungo huyo kushindwa kuichezea timu yake kwenye mchezo wa kwanza wa michuano hiyo kwa timu hii .

Yaya Toure akitazamwa na daktari wa timu na kocha wake Herve Renard baada ya kuumia kwenye mazoezi ya kwanza nchini Equatorial Guinea.
Ivory Coast ilianza rasmi mazoezi yake hapo jana na wanatarajiwa kufungua kampeni yao ya Afcon kwa mchezo wa kundi D utakaopigwa kesho kutwa jumanne dhidi ya Guinea .
Bado haijafahamika kama Toure ataweza kufanya mazoezi kwa siku zilizosalia kabla ya mchezo na haijaweza kufahamika kama atakuwepo wakati Ivory Coast ikicheza na Guinea .
No comments:
Post a Comment