WFP kupunguza msaada wa chakula Uganda - LEKULE

Breaking

27 Jan 2015

WFP kupunguza msaada wa chakula Uganda

 Shirika la chakula duniani WFP limetangaza kuwa litapunguza kwa nusu kiwango chake cha msaada wa chakula kwa takriban wakimbizi 150,000 nchini Uganda.
Shirika hilo limesema kuwa linakabiliwa na ugumu kuchangisha dola millioni 30 zaidi ili kufadhili shughuli zake nchini Uganda kwa kipindi cha miezi sita ijayo.
WFP limeelezea hatua hiyo kama ya mwisho iliolenga kuhakikisha kwamba watu walio katika mazingira magumu bado watapokea msaada.
Limesema kwamba litaendelea kutoa chakula kwa makumi ya maelfu ya wakimbizi ambao wametoroka vita katika taifa jirani la Sudan Kusini

No comments: