Hoteli yashambuliwa Tripoli, Libya - LEKULE

Breaking

27 Jan 2015

Hoteli yashambuliwa Tripoli, Libya



Watu wenye silaha wameshambulia hoteli moja maarufu kufikiwa na wageni kutoka nje katika mji mkuu wa Libya, Tripoli, na kuua walinzi watatu na watu wengine 12 kujeruhiwa.

Watu kadha wenye silaha walivamia hoteli ya Corinthia mjini Tripoli na kufyatua risasi katika eneo la mapokezi. Bomu lililokuwa limetegwa katika gari lililipuka nje ya hoteli.

Baadhi ya watu wenye silaha bado wanasadikika kuwa wako ndani ya hoteli. Haifahamiki kama wafanyakazi au wageni wangali katika hoteli hiyo.

Mgeni mmoja raia wa Ufilipino, alikuwa miongoni mwa majeruhi wa tukio hilo.

Akaunti moja ya mtandao wa twitter inayohusishwa na na kikundi cha Islamic State imesema kundi hilo limeshambulia hoteli hiyo. Madai hayo hayajathibitishwa.

Raia mmoja waliyeshuhudia shambulio hilo ameiambia BBC: "ghafla nilisikia milio ya risasi na kuona watu wakikimbia kuja upande wangu, na wote tulitoroka kupitia nyuma ya hoteli kupitia njia ya chini ya gereji."

Jumla ya washambuliaji haifahamiki. Vyanzo mbalimbali katika eneo la tukio vinasema kulikuwa na washambuliaji kati ya watatu na watano.

Habari za ulama zimeiambia BBC kuwa mtu mmoja mwenye silaha amekamatwa na washambuliaji wengine wawili bado wako ndani ya hoteli.

Majeshi ya usalama yamekusanyika kuzunguka hoteli kufuatia mlipuko na mwandishi wa BBC Rana Jawad aliyeko mjini Tripoli anasema eneo kuzunguka hoteli hiyo limefungwa.

No comments: