Mahakama moja nchini Ufaransa imewazuia wazazi kumpatia jina la Nutella mwana wao wa kike, ikisema kuwa jina hilo litamfanya azomwe ama hata kochokozwa.
Jaji wa mahakama hiyo badala yake aliagiza aitwe Ella.
Alisema katika uamuzi wake kwamba jina Nutella ni jina linalotumiwa na mafuta yanayotumiwa kupaka mkate.
Ni kinyume na maslahi ya mtoto ambapo jina hilo litamfanya kuchokozwa ama hata kuzomwa'',alisema.
Wazazi nchini Ufaransa huwa wako huru kuchagua majina ya watoto wao ,lakini viongozi wa mashtaka wana haki kuripoti kile wanachoona kuwa sio majina mazuri.
Wazazi wa kesi hiyo hawakuwasili mahakamani ili kusikilizwa kwa kesi yaomkwa hivyo jaji huyo aliamuru kwamba jina Ella ndio jina zuri kupewa msichana huyo.
Kumekuwa na msururu wa kesi zinazohusu majina ya watoto Ufaransa tangu 1993, wakati wazazi walipopewa huru kuwataja majina waliotaka.
No comments:
Post a Comment