Kocha wa Senegal aishtumu West Ham - LEKULE

Breaking

27 Jan 2015

Kocha wa Senegal aishtumu West Ham

Kocha wa Senegal Alain Giresse aishtumu West Ham



Klabu ya West Ham ilionyesha mfano m'baya kwa kumchezesha mshambuliaji Diafra Sakho wikendi iliopita kulingana na kocha wa Senegal Alain Giresse.

Sakho mwenye umri wa miaka 25 alijiondoa katika kikosi cha Senegal cha kombe la mataifa ya Afrika mapema mwezi hutokana na jeraha la mgongo,lakini akaichezea kilabu ya West ham siku ya jumapili.

''Iwapo huwezi kusafiri kwa wiki sita na mara ghafla unacheza soka,basi kuna dawa ya miujiza Uingereza'',alisema Giresse.



''Nimeshangaa kugundua kwamba alicheza .

Sakho alikuwa amechaguliwa katika kikosi cha watu 23 cha timu ya Senegal kabla ya kujiondoa kabla ya michuano ya kombe hilo ilioanza januari 17.

No comments: