Utata kuhusu shahidi wa ICC Kenya - LEKULE

Breaking

14 Jan 2015

Utata kuhusu shahidi wa ICC Kenya

Familia ya Yebei ilimtambua kama yeye iihali polisi wanasema alama za vidole zinamuonyesha maiti kuwa Yusuf Hussein



Afisaa mmoja wa polisi nchini Kenya amesema kwamba alama za vidole za mtu aliyeuawa na kutumbukizwa ndani ya mto hazionyesi kuwa za mtu ambaye mawakili wa mahakama ya kimataifa ya ICC walisema ni shahidi wa mahakama hio aliyetoweka.

Mtu huyo aliyetajwa kuwa Meshack Yebei alisemekana kuwa shahidi wa naibu Rais wa Kenya William Ruto ambaye anakabiliwa na tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama hio.

Afisaa huyo John Kariuki, aliambia wandishi wa habari Jumatano kwamba, alama za vidole zilizotolewa kwa maiti hio zinazoonyesha kuwa za Yusuf Hussein na wala sio Meshack Yebei shahidi wa ICC ambaye ametoweka.

Familia ya Yebei ilikuwa imetambua mwili huo kama wa jamaa wao lakini sasa kumeibuka utata kuhusu mtu huyo.

Wakili wa Naibu Rais William Ruto,Karim Khan amesema kwamba Yebei alitoweka Disemba tarehe 28 na alikuwa shahidi wa upande wa utetezi.

Bwana Ruto pamoja na mtangazaji Joshua Sang wamefikishwa ICC kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/8 ambapo zaidi ya watu 1,000 waliuawa.

No comments: