Ongwen akabidhiwa kwa wanajeshi wa UGANDA - LEKULE

Breaking

14 Jan 2015

Ongwen akabidhiwa kwa wanajeshi wa UGANDA


Kamanda mkuu wa kundi la waasi la LRA nchini Uganda, aliyejisalimisha wiki jana, Dominic Ongwen , amekabidhiwa kwa wanajeshi wa Uganda walio katika Jamuhuri ya Afrika ya kati.
Muasi huyo, Dominic Ongwen, anasemekana kuwa naibu kiongozi wa kundi hilo Joseph Kony na alikamatwa na wanajeshi wa Marekani wiki jana ingawa waasi wa Seleka wanasema wao ndio waliomkamata.
Waasi hao walisema kwamba walimkatama Ongwen baada ya makabiliano ya muda ingawa jeshi la Marekani lilisitiza kuwa alijisalimisha na tangu hao wamekuwa wakimzuilia.
Uganda imesema kwamba itamkabidhi kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, ambako anatakikana kwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu.
Kundi la LRA liliwateka nyara wasichana na wavulana huku wavulana wakilazimishwa kuwa wapiganaji na wasichana wakifanywa watumwa wa ngono.
Ongwen pamoja na Joseph Kony wanatakikana na mahakama ya ICC kujibu tuhuma za kutenda uhalifu dhidi ya binadamu.
Je Ongwen ni nani?
-Inaarifiwa alitekwa nyara na waasi wa LRA akiwa na umri wa miaka 10 wakati alipokuwa anaelekea shuleni Kaskazini mwa Uganda.
-Miaka iliyofuata, alipanda ngazi na kuwa kamanda
-Anatuhumiwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu ikiwemo, kuwatumia watoto kama watumwa.
-ICC ilitoa kibali cha kumkamata mnamo mwaka 2005.
-Kuliwa na madai kwamba aliuawa katika mwaka 2013 ambapo Marekani ilitangaza ahadi ya zawadi kwa yeyeote mwenye taarifa kumhusu.

No comments: