Umoja wa Ulaya wataka kudumishwa amani Misri - LEKULE

Breaking

26 Jan 2015

Umoja wa Ulaya wataka kudumishwa amani Misri




Umoja wa Ulaya umezitaka pande zote zinazozozana huko Misri kudumisha amani nchini humo. Federica Mogherini mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya ameashiria utumiaji nguvu za ziada na kuuawa raia kadhaa wa Misri katika mapigano ya hivi karibuni na kusisitiza juu ya ulazima wa kufanyika kwa amani maandamano nchini humo.

Mogherini amezitaka pande zote zinazozozana huko Misri kufanya mazungumzo kama njia pekee itakayoweza kutatua mgogoro wa nchi hiyo na kudumisha amani nchini. Mikoa na miji mbalimbali ya Misri jana ilishuhudia mapigano na utumiaji mabavu katika kuadhimisha mwaka wa nne tangu kujiri mapinduzi ya wananchi ya tarehe 25 Januari yaliyomng’oa madarakni dikteta wa nchi hiyo Hosni Mubarak mwaka 2011. Watu zaidi ya 20 wakiwemo polisi watatu waliuawa jana wengine 82 kujeruhiwa katika vurugu za jana huko Misri. 

No comments: