Steven Gerrard kuihama Liverpool - LEKULE

Breaking

2 Jan 2015

Steven Gerrard kuihama Liverpool

Nahodha wa timu ya Liverpool ya Uingereza Steven Gerrard ataondoka katika klabu hiyo wakati mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu.

Gerrard, mwenye umri wa 34, alikuwa huru kusaini makataba wa awali na timu ya nje siku ya Alhamisi na anaaminika kutatakiwa na vilabu vya Marekani.

Gerrard, ambaye alianza kuichezea Liverpool mwaka1998, hatahamia katika klabu nyingine ya Uingereza.

Liverpool ilimpa Gerrard mkataba mpya mwezi Novemba na atatoa taarifa kuhusu mustakhabali wa maisha yake ya soka Ijumaa.

Rais wa klabu ya LA Galaxy ya Marekani Chris Klein amekataa kusema lolote kuhusu klabu yake kumsajili Gerrard, ambaye alifunga penalti mbili katika matokeo ya sare ya 2-2 na timu ya Leicester City katika mechi iliyochezwa siku ya Mwaka Mpya 2015.

No comments: