Chelsea yapewa kichapo na Totenham - LEKULE

Breaking

2 Jan 2015

Chelsea yapewa kichapo na Totenham

Chelsea ilicharazwa na kilabu ya Totenham na hivyobasi kusalimu amri ya uongozi wa ligi ya Uingereza.

Bao la Diego Coasta liliiweka mbele Chelsea ,lakini bao la Kane lilisawazisha mambo na kuwa 1-1 kabla ya Danny Rose kuiongezea bao la pili Totenham.

Kane aliangushwa na Gary Cahil kabla ya Andre Townsend kufunga kupitia mkwaju wa penalti.

Kane baadaye alifunga bao la nne kunapo dakika ya 52.

Mkwaju wa Eden Hazard katika dakika ya 61 uliipatia Chelsea matumaini lakini Nacer Chadli alifanya mambo kuwa 5-2 kabla ya John Terry kuipatia bao la tatu na la kufutia machozi Chelsea.

Bao hilo la Terry sasa linaziweka Chelsea na Manchester City katika nafasi ya kwanza zote zikiwa na mabao sawa na alama sawa.

Iwapo timu hizo zitakuwa sawa kama ilivyo sasa mwishoni mwa msimu huu basi zitalazimika kucheza kati yao ili kutoa mshindi.

Mnamo mwezi Novemba 22,Chelsea ilikuwa na uongozi wa alama nane dhidi ya City,kabla ya kushindwa mara mbili na kupata sare mara mbili.

No comments: