Polisi wawili nchini Rwanda,
wamefungwa miaka 20 jela kwa kumuua mwanaharakati wa kupinga ufisadi,
aliyekuwa anachunguza kashfa ya ulanguzi wa madini mpakani.
Gustave
Makonene, aliyekuwa anafanya kazi na shirika la kimataifa la
Transparency International, aliuawa Julai 2013 mjini Rubavu karibu na
mpaka na DRC.Viongozi wa mashitaka walisema kwamba watuhumiwa walimuua mwanaharakati huyo baada ya kugundua kuwa alikuwa na taarifa kuhusu biashara yao haramu ya madini.
Hata hivyo Transparency International imesema kuwa adhabu hiyo haitoshi.
Jaji alisema kuwa wawili hao Nelson Iyakaremye na Isaac Ndabarinze hawakupata kifungo cha maisha kwani walikiri makosa na kushirikiana na polisi kwa uchunguzi.
Eneo la Congo Mashariki lina utajiri mkubwa wa madini , nyingi ambayo hutumiwa kutengeza komputa na simu za mkononi. Madini hayo ndio yamechochea vita nchini humo.
Ufadhili wa kundi la wasi wa M23 ulidaiwa kutokana na biashara haramu ya madini ambayo huuzwa nchini Rwanda.
Jeshi la Congo, pamoja na kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa, walishirikiana kupambana na waasi hao na kuwatimua mwaka 2013 huku Rwanda daima ikikanusha madai ya kufadhili waasi hao.
No comments:
Post a Comment