Mwili wake ulipelekwa msikitini kuswaliwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Riyadh kabla ya kuzikwa
Viongozi kadhaa wa nchi za kiarabu na marafiki za Asudi Arabia walihudhuria mazishi hayo.
Awali mfamle mpya nchini Saudi Arabia Salman bin Abdul-Aziz al Saud alisema kuwa ataendeleza sera za mtangulizi wake ambaye aliaga dunia jana alhamis baada ya kuugua ugonwa wa nimonia.
Katika hotuba iliyotolewa kupitia kituo cha runinga cha taifa mfalme huyo pia alitoa wito wa kutaka kuwepo amani miongoni wa nchi za kiarabu.
Wizara muhimu zikiwemo ya mambo ya kigeni, mafuta na fedha hazijafanyiwa mabadliko .
Wizara wa ulinzi ambayo awali ilikuwa inasimamiwa na mfalme mpya itaongozwa na mwanawe wa kiume Mohammed bin Salman.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa Saudi Arabia inakabiliwa na chamgamoto nyingi zikiwemo tishio la kundi la wanamgambo wa Islamic State .
Mfalme Abdullah amerithiwa na kakake, Salman, aliye na umri wa miaka 79. Mfalme Abdullah aliingia uongozini mnamo mwaka 2005 alipomrithi nduguye mwingine, Fahad. Hata hivyo tayari alitarajiwa kuwa kiongozi wa Saudia kwa muda wa miaka kumi kwa sababu mfalme aliyemtangulia alikuwa anaugua kiharusi.
Viongozi wengi wa dunia wametuma risala za rambi rambi kwa utawala wa Saudia kufuatia kifo cha mfalme wao Abdullah.
Nchi kama vile Bahrain na Jordan zimetangaza siku arobaini za maombolezi kwa heshima yake.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon, amempongeza mflame huyo kwa juhudi zake za kutafuta amani katika mashariki ya kati.
Japo mfalme Abdullah amesifiwa ndani ya nchi yake na hata baadhi nje ya nchi, wanaharakati wa haki za binadamu wamejitokeza kukashifu utawala wake wakisema kuwa alileta mabadiliko machache sana ya kusifika.
Saudi Arabia ina ushawishi mkubwa katika mataifa ya Pakistan, Bangladesh na India ambapo inafadhili miradi kadha na shule nyingi zinazotoa mafunzo ya kidini.
Makundi nchini pakistan kwa muda mrefu yamekuwa yakishutumu baadhi ya shule hizo ambazo yanasema zinaendesha kampeni za chuki dhidi ya Washia
Chamgamoto inayomkabili mfalme huyo mpya ni kuhakikisha kuwa msaada wa mamilioni ya ya dola hauwafikii wale wanaounga mkono chuki.
Makundi ya haki za binadamu yanaamini kuwa uongozi mpya wa saudi Arabia utatekeleza ahadi za muda mrefu za kuboresha mazingira kwa mamilioni ya wafanyikazi wahamiaji kutoka nchi za Asia.
Wanasema kuwa hadi sasa waajiri nchini Saudi Arabia wana usemi mkubwa juu wa wajiriwa wao.
No comments:
Post a Comment