Mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC imempa kiongozi wa mashtaka katika mahakama hiyo Fatou Bensouda makataa ya juma moja kutoa ushahidi dhidi ya rais wa kenya la sivyo aondoe mashtaka dhidi yake.
''Kucheleweshwa kwa kesi hiyo ya rais Uhuru ni kinyume na maslahi ya haki ''iliamua.
Rais Kenyatta ni kiongozi wa kwanza wa taifa kufika katika mahakama hiyo tangu ashtakiwe rasmi mwaka 2012 na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu,ambayo ameyakana.
Kiongozi huyo wa mashtaka ametaka kupewa mda zaidi ili kujenga kesi yake dhidi ya kiongozi huyo.
Anasema kwamba mashahidi wamehongwa na kutishiwa huku serikali ya Kenya ikikataa kutoa stakhabadhi muhimu za kesi hiyo.
Bwana Kenyatta amekanusha kuchochea ghasia kufuatia mgogoro wa uchaguzi wa mwaka 2007 ili kumpatia ushindi aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki na kusema kuwa kesi hiyo ni ya kisiasa.
Akikataa ombi la kiongozi huyo wa mashtaka kuchelewesha kesi hiyo, majaji wa mahakama hiyo walisema kuwa wamempatia wiki moja Bensouda kusema iwapo ataitupilia mbali kesi hiyo ama ushahidi alio nao unaweza kuhimili kesi hiyo kuendelea.
Rais Kenyatta alishinda uchaguzi wa urais mwaka 2013 kupitia usaidizi wa Mwai Kibaki.
Aliitumia kesi hiyo kutafuta kuungwa mkono huku akiikashifu mahakama hiyo ya mjini Hague kwa kuingilia maswala ya Kenya.
Ameshtakiwa na mahakama hiyo kwa kuhusika moja kwa moja katika mauaji ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008.
Takriban watu 1200 waliuawa katika ghasia hizo huku wengine 600,000 wakiwachwa bila makao.
No comments:
Post a Comment