Vita Simba,Yanga na Mbeya City. - LEKULE

Breaking

21 Nov 2014

Vita Simba,Yanga na Mbeya City.


Klabu za Simba na Yanga zimeingia kwenye vita kubwa ya kumsajili winga na kiungo mshambuliaji wa pembeni wa Mbeya City Deus Kaseke .
Kaseke aliingia jijini Dar-es-salaam wiki hii ambako aliletwa na viongozi wa Simba ambao walianza kufanya naye mazungumzo .
Kaseke alikubali kujiunga na Simba kwa sharti la kulipwa ada ya uhamisho ya shilingi milioni 40 huku Simba wakiwa tayari kutoa milioni 20
  Sinema hii ya kumsajili Kaseke iliingia kwenye hatua tamu zaidi baada ya kuwepo kwa ripoti ya mchezaji huyo ‘kutekwa’ na watu wa Yanga ambao walikuwa wanataka kumsainisha mchezaji huyo kwenye klabu yao .
Kaseke hadi sasa amerudi nyumbani kwao huko Mbeya na timu yoyote itakayokuwa na nia ya kumsajili italazimika kufunga safari na kumfuata huko .
       Taarifa nyingine zinadai kuwa Yanga imemtuma mchezaji wake wa zamani ambaye ni kiongozi kwenye klabu hiyo kwenda jijini Mbeya kukamilisha mazungumzo ya usajili wa Deus Kaseke .
Endapo Mbya City itampoteza Kaseke huenda ikawa hatarini kuendelea na mfululizo wa matokeo mabaya ambayo wamekuwa wakiyapata kwani hakuna asiyefahamu kuwa mchezaji huyo ni muhimu kwa klabu hiyo .

No comments: