Staa wa Bongo Fleva aliyeyatoa ya moyoni baada ya kufanyiwa dhuluma, - LEKULE

Breaking

21 Nov 2014

Staa wa Bongo Fleva aliyeyatoa ya moyoni baada ya kufanyiwa dhuluma,

huyu pichan juu ndiye mlalamikiwa.

Tumeshazoea kwamba mtu anapokufanyia ubaya basi lazima na wewe ulipize ubaya ni watu kadhaa ufanya hivyo baada ya kukerwa na ulichofanyiwa.
Mkali wa hit single ya Wema kwa Ubaya ‘Linex Sunday Mjeda’ Nov 21 kupitia ukurasa wake wa Facebook alipost ujumbe na picha ya mtu anayesadikiwa kumdhuluma fedha.Huu ndio ujumbe wake ‘Mnamo miezi ya kwanza mwaka huu jamaa huyu pichani aliniunizia gari m11 nikaa nalo siku mbili nikagundua halifanani na pesa yangu nikaamua kurirudisha aliyenikutanisha na jamaa huyu ni msanii mwenzangu Steve Nyerere mi ni kijana ambaye napata pesa kwa njia zinazokubalika kwenye jamii nimedai sana mpaka nimechoka kila siku nazungushwa kwa kua sijawahi kumchukulia MTU RB wala kumuweka police mtu nimekata tamaa si kwamba nna pesa nyingi lakini nimeamua kumuachia Mungu na kuanzia Leo sitamsumbua na nimeamua kusamehe najua kuna watu mtaniona mjinga lakini mi nimefuata kile moyo wangu unachotaka namuombea Maisha mema lakini siku akikumbuka kuna jasho la mvuja jasho aliwahi kuchukua Asinisahau Nawaombea yeye na Steve Nyerere Maisha mema na waishi kwa amani kabisa asanteni kwa ushauri mlionipa insta na mpaka baadhi ya wanasheria kujitokeza kunisaidia tatizo langu for free Tanx’Aliandika

No comments: