SWAPO yaelekea kushinda tena Namibia - LEKULE

Breaking

29 Nov 2014

SWAPO yaelekea kushinda tena Namibia


 Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi mkuu wa Namibia yanaonesha kuwa chama tawala cha SWAPO kimeshinda kwa kura nyingi.

SWAPO imetawala Namibia tangu nchi hiyo kupata uhuru mwaka wa 1990.

Lakini wanasaiasa wa upinzani kwa mara nyengine tena wanataka kura ibatilishwe, wakidai kuwa kanuni zilikiukwa na wapigaji kura waliendelea kupiga kura hata baada ya muda uliowekwa.

Mahakama makuu katika mji mkuu, Windhoek, yalitupilia mbali madai ya kuahirisha uchaguzi uliofanywa Ijumaa.

Wanasiasa wa upinzani wanasema upigaji kura wa digitali, bila ya kutumia karatasi, unatoa fursa ya kufanya udanganyifu.

Tume ya uchaguzi imekiri kuwa kulitokea matatizo kwenye mashini wakati wa kupiga kura, hata hivyo inasema matokeo yatakuwa ya kuaminika.

No comments: